KAMATI YA UFUNDI YAKUTANA KUPITIA NYARAKA MBALIMBALI

27 Oct, 2022
Kamati ya ufundi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo Oktoba 27, 2022 imekaa kupitia nyaraka mbalimbali zinazoihusu kamati hiyo ikiwemo vigezo vya kusajili taasisi mbalimbali za michezo pamoja katiba, kwa lengo la kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya michezo.
Kamati hiyo imemhusisha Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo ambayo ndiye Mwenyekiti wa kamati, Halima Bushiri Katibu na wajumbe Riziki Majala, Ameir Mohamed na Allen Alex.