KATIBU MSTAAFU WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI (CISM) KANALI DORAH MAMBY KOITA AKUTANA NA WATENDAJI WA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA(BMT)
service image
12 Oct, 2022

Katibu Mstaafu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) Kanali Dorah Mamby Koita, akiambatana na Mkurungenzi wa Michezo ya CISM nchini Tanzania Kanali Joseph Bakari, leo tarehe 12 Oktoba 2022 wamekutana na baadhi ya watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kwa lengo la kujadili namna ya kushirikiana kutekeleza dhamira mbalimbali za Shirikisho la Michezo ya Majeshi ya Afrika (OSMA) ikiwa ni pamoja na kuhimiza Mataifa ya kiafrika kuwa wanachama hai wa OSMA na CISM na kujitolea kuwa wenyeji wa michezo na mashindano mbalimbali ya kijeshi yanayoandaliwa na mashirikisho hayo.

Ziara hiyo pia ililenga kujadili namna ya kutumia shughuli za michezo na utimamu wa mwili baina ya Majeshi ya nchi wanachama Barani Afrika kama njia muhimu ya kueneza Amani duniani badala ya vita na hivyo kuwa kichocheo muhimu katika maendeleo ya uchumi.