NSC EXECUTIVE SECRETARY MEETS WITH TPBRC TRANSITION LEADERSHIP

02 Sep, 2025
Katibu Mtendaji wa BMT, Bi. Neema Msitha mapema leo Septemba 02, 2025 Ofisini kwake, amekutana na Uongozi wa mpito wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) walioteuliwa Agosti 14, 2025 na Mhe. Waziri mwenye dhamana ya michezo Prof. Paramagamba Kabudi kwa lengo la kuwapa mwongozo wa majukumu waliyokasimiwa ili wayatekeleze kwa muda uliokusudiwa.
Wajumbe wa Kamati hao wameongozwa na Mwenyekiti Patrick Nyembela, Makamu Mwenyekiti Jackobu Mbuya, Katibu Gordon Nsajigwa, na Mjumbe Shafii Dauda na wengine ambao hawakufika ni Bi. Irene Mwasanga na Ibrahim Kamwe.