KILELE CHA MBIO ZA MWENGE
service image
14 Oct, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kagera wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, hitimisho la maonesho ya wiki ya vijana kitaifa pamoja na kumbukumbu ya kifo cha Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Nyerere.

Hayo yamefanyika kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera tarehe 14 Oktoba, 2022.