Ladies First 2023
service image
26 Nov, 2023

Unguja Kusini watetea ubingwa wao msimu wa tano Ladies First
Mkoa wa Kusini Unguja imefanikiwa kutetea ubingwa wake katika mashindano ya Wanawake 'Ikangaa Ladies First' yaliyomalizika Novemba 26, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Kusini Unguja imeongoza kwa medali nne za dhahabu, moja ya fedha hivyo amejikusanyia medali tano, akifuatiwa na Kilimanjaro akiwa na medali za dhahabu tatu, fedha mbili na Shaba Tano hivyo amejikusanyia medali 10 na Pwani akimalizia nafasi ya tatu.

Akizungumza baada kumalizika kwa mashindano hayo Kocha Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja, Makame Hassan, ametaja kujituma mazoezi ndio siri kubwa ya ushindi huo mfululizo.

Wakati huo huo matokeo ya mchezaji mmoja mmoja katika mita 100 Winfrida Makenji kutoka Kusini Unguja amekimbia muda wa 11:59, akifuatiwa na Elizabeth Victor amekimbia muda wa 12:13 na Bertha Andrew amekimbia muda 12: 28 wa Kilimanjaro.

Matokeo mengine mita 200 Winfrida Makenji wa kusini Unguja ameongoza kwa kukimbia 24:50, huku Jane Maige wa Mjini Magaharibi akishika nafasi ya pili Kwa kukimbia 25:61 na watatu Bertha Andrew wa kilimanjaro akikimbia 25:99.

Katika mita 400 Merciana John wa Pwani amekimbia muda wa 59:19, huku Thereza Benald wa kusini Unguja amekimbia 59:93, akimaliza nafasi ya tatu Grace Charles wa Tabora amekimbia 61:34.

Kwa mita 800 Elizabeth Boniface wa Kilimanjaro amekimbia 2:14:71 huku Salma Charles wa Pwani amekimbia 2:15:27 na Zahara Ramadhan wa Singida amekimbia 2:19:75.

Mita 1500 Hamida Mussa wa Kilimanjaro ameongoza kwa kukimbia saa 4:39:44, akifuatiwa na Elizabeth Boniphace wa Kilimanjaro amekimbia saa 4:40:69 na Zainabu Issa wa Pwani ameshika nafasi ya tatu amekimbia saa 4:45:47.

Aidha katika mita 5000 Elizabeth Ilanda wa Kilimanjaro ameongoza kwa kukimbia 17:39:46, huku Neema Sanka wa Manyara 18:03:22 na Neema Nyaisawa wa Kilimanjaro amekimbia 18:04:08.