MASHINDANO YA POOLTABLE
service image
14 Aug, 2023

KLABU ya Tip top ya Jijini Dar es salaam imefanikiwa kutawazwa kuwa Ubingwa wa Mashindano ya wazi ya pooltable ya kusherekea sikukuu ya nanenane (88 Grand open Pool Competition) yaliyoisha tarehe 13 Agosti, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Klabu hiyo imefanikiwa kupata Kombe, fedha taslimu 500,000 na medali, huku Vegas ikikamata nafasi ya pili ikipata fedha na medali na aliyekuwa bingwa wa mwaka 2022 sniper ilimalizia nafasi ya tatu.



Kwa mshindi wa mchezaji mmoja mmoja kwa wanaume nafasi ya kwanza hadi ya tatu zilichukuliwa na wachezaji kutoka Klabu ya Tip top, ikiwamo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Abdul Saidi Kiande ambaye ni mchezaji bora wa Mashindano hayo huku nafasi ya pili ikienda Kwa Festo Richard na Said Emmanuel akimalizia nafasi ya tatu.


Kwa Upande wa wanawake Bingwa mtetezi Jackline Tido kutoka Dodoma amefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mara Nyingine, uku Judith Machafuko akishika nafasi ya pili.



Akizungumza baada ya kumalizika kwa mashindano hayo Nahodha wa Klabu ya Tip top Festo Richard, alitaja mazoezi na nidhamu ya kumheshimu mpinzani wanaliokuwa wanapambana naye ndio siri kubwa ya mafanikio ya kutwaa ubingwa huo .

Alisema kuwa mchezo ulikuwa mzuri na changamoto za ushindani zilikuwa kubwa kutokana kila mmoja alikuja amejiandaa kufanya vizuri.

"Tunashukuru Mungu kwa hili na pia viongozi wetu kwa kutuunga mkono kwa maandalizi na t kutawazwa Mabingwa," alisema Richard .

Kwa Upande Mwenyekiti wa Chama cha Pooltable Tanzania (TAPA) Wilfred Makamba, aliwapongeza Mabingwa na washiriki wote na kuwataka kujiandaa zaidi kwa ajili ya mashindano mengine.

"Pongezi kwa mabingwa wameonyesha ushindani katika Michezo yao na wamepata ushindi kwa haki, lakini washiriki wengine wamejitoa walichokifanya na sisi viongozi tupo nyuma yao kwa kuwashika mkono," alisema Makamba

Mashindano hayo yalishirikisha wachezaji kutoka mikoa ya Mbeya, Morogoro, Iringa, Manyara, Dodoma, Mbeya, Zanzibar na wenyeji Dar Es Salaam.