MICHEZO NI FURSA KWA VIJANA
service image
11 Oct, 2022


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amefafanuliwa fursa mbalimbali zinapatikana kwa vijana kupitia michezo.

Prof. Ndalichako amefafanuliwa fursa hizo tarehe 11 Oktoba, 2022 na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Baraza la michezo la Taifa (BMT) Najaha Bakari wakati alipotembelea maonesho ya wiki ya vijana kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Gymkhana Mkoani Kagera.

"Michezo ni afya, ajira na huleta mahusiano mazuri sehemu tofauti ikiwemo maofisini,"alisema Najaha.

Maonyesho ya wiki ya Vijana Kitaifa yameanza tarehe 08 na yatahitimishwa tarehe 14 Oktoba siku ya kumbukumbu ya kifo cha Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwl.Julius Nyerere na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru.