MKUU WA WILAYA YA UBUNGO MHESHIMIWA HERRY JAMES AMEZINDUWA MASHINDANO YA MSIMU WA NNE YA GOBA HILL MARATHON 2023

Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Herry James tarehe 14 Oktoba, 2022 amezinduwa mashindano ya msimu wa nne ya Goba Hill Marathon 2023,uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Joy Goba jijini Dar es Salaam, ambapo amesema lengo la mashindano hayo ni kuchangia afya ya mama na mtoto hususani kwa hospital zilizopo maeneo ya Goba.
" Kwa niaba ya serikali nawashukuru waandaaji, kwani msingi wa jambo hili ni kuleta umoja na kujenga afya zetu lakini kipekee kitakachopatikana kinakwenda kuchochea huduma ya kijamii katika eneo letu.
Aidha Mhe. James amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kutoa ushirikiano kwa makundi mbalimbali katika kuhakikisha michezo inaleta ajira.
Naye Afisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Charles Maguzu amewataka watanzania wengi kujitokeza kushiriki mbio kwakuwa kutaimarisha afya zao.