MSITHA AONGOZA MAZOEZI YA VIUNGO TANZANITE 2022

22 Oct, 2022
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha ameshiriki katika mbio za polepole pamoja na mazoezi ya viungo kuendelea kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo.
Matukio hayo yamefanyika leo asubuhi Oktoba 22 ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya tamashà la kimataifa la michezo ya wanawake ambalo linafikia tamati leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.