NGUMI YAMUHAKIKISHIA RAISI SAMIA NA TAIFA LA TANZANIA MEDALI YA PILI BAADA YA USHINDI WA EZRA PAULO
service image
19 Mar, 2024

Tanzania yajihakikishia medali ya pili katika michezo ya Afrika Accra 2023 inayoendelea nchini Ghana baada ya askari wake wa pili wa Kikosi cha Faru Weusi wa Ngorongoro EZRA PAULO MWANJWANGO kushinda pambano lake la robo fainali dhidi ya Mujinga Frazier kutoka DR Congo kwa points 5-0.

Ilikuwa katika pambano namba 74, uzani wa Lightweight 60kg lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Bukom Arena ambapo bondia wetu Ezra Paulo alicheza kwa ustadi wa hali ya juu na kuwashawishi majaji wote 5 kumpatia ushindi na kuingia hatua ya Nusu Fainali.

Ezra sasa anakua bondia wa pili kuihakikishia Tanzania kupata medali ya pili katika michezo hii ya 13 ya Afrika Accra 2023 inayoendelea katika Jiji la Accra, Ghana na sasa atacheza hatua ya nusu fainali dhidi ya Andrew Chilata kutoka Zambia.

Bondia wa kwanza kuihakikishia Tanzania medali ni Musa Maregesi wa uzani wa Cruiserweight 86 ambaye tayari yuko hatua ya nusu fainali.