KUFUZU OLIMPIKI: CHANGALAWE APOTEZA KWA POINTI DHIDI YA MNORWAY

09 Mar, 2024
Jana ilikua siku mbaya kazini kwa bondia tegemeo wa Taifa Yusuf Changalawe baada ya kupoteza kwa maamuzi ya kutofautisha *(Split decision)* ambapo majaji 3 dhidi ya 2 walimpa ushindi mpinzani wake Mindaugas Gedminas kutoka nchini Norway.
Kwa matokeo hayo ya kupoteza kwa pointi 3-2 ni rasmi Changalawe amehitimisha safari yake katika mashindano haya ya kwanza ya Dunia ya kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024. Alikua amebakisha mapambano 2 kushinda ili aweze kufuzu.
Changalawe anatarajiwa kuondoka Milano, Italy wakati wowote kuelekea Accra, Ghana kuungana na wenzake 7 kushiriki mashindano ya Afrika Accra 2023 ambapo ngumi zitaanza rasmi kupiganwa tarehe 14-03-2024.