PONGEZI KWA IZMIR
service image
10 Mar, 2022

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) linatoa pongezi kwa mchezaji Shedrack Hebron aliyechaguliwa kujiunga na klabu ya Yeditepe mjini Istanbul kwenda kucheza Soka la kulipwa kwa watu wenye ulemavu.

Shedrack anakuwa mchezaji wa pili wa timu ya Taifa ya mpira wa Miguu kwa watu wenye ulemavu (Tembo Warriors) kwenda nchini Uturuki baada ya mchezaji wa kwanza Frank Ngailo kupata usajili katika klabu ya Izmir.