SERIKALI INAPAMBANA KUTAFUTA WADHAMINI
service image
20 Jul, 2023

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu, amesema Serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha zinapata udhamini mkubwa kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Alisema tayari mashiriki ya kimataifa likiwamo Shirika la kazi duniani (ILO) na Benki ya Dunia na wengine ambapo baadhi wanatarajia kusaini makubaliano ya kusaidia timu za taifa zinazoshiriki kimataifa.

Hayo ameyasema tarehe 20 Julai, 2023 wakati alipombatana na Waziri mwenye dhamana na Wizara ya michezo Balozi Dkt.Pindi Chana katika hafla ya kufunga mafunzo kwa viongozi wa vyama vya michezo na uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa vyama vya michezo wa kidigitali, tukio lililoratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Jijini Dar es salaam.