SHAMRASHARA ZA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA VIJANA
service image
12 Oct, 2022

Shamrashara za uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya vijana zikiendelea katika viwanja vya Gymkhana Mkoani Kagera leo Oktoba 12, 2022, huku Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ndiye Mgeni rasmi katika tukio hilo adhimu kwa vijana.



Aidha, maadhimisho hayo yanatarajiwa kufungwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan tarehe 14 Oktoba Mkoani hapo siku ya kumbukizi ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Nyerere pamoja na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru.