SIMBU AIBUKA KINARA MBIO ZA UBINGWA WA DUNIA KWA WANAUME
                            
                                
                                     15 Sep, 2025
                                
                            
                            Mwanariadha Alphonce Felix Simbu ashinda mbio za riadha za dunia ambazo zinafanyika jijini Tokyo, nchini Japani na kumshinda mpinzani wake kwa tofauti ya sekunde 0.03 ambaye ni mwanariadha kutoka Ujerumani Amanol Petros
Alphone Simbu ameshinda mbio za dunia kwa kukimbia kwa saa 2:09:48 na kufanikiwa kupata medali ya kwanza ya dhahabu kwa Tanzania katika mashindano ya dunia ya Tokyo 2025 .

