Kliniki ya Michezo

03 Sep, 2025
Serikali ya Tanzania imeishukuru Serikali ya Marekani kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Michezo ambayo ni sekta nyeti inayokusanya Vijana wengi na kutoa ajira kwa Makundi Tofauti.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 3 Septemba, 2025 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa BMT, Bi. Neema Msitha wakati wa zoezi la kuhitimisha kliniki ya mchezo wa Soka kwa vijana na Mchezo wa Goal Ball kwa watu wenye ulemavu wa macho ambayo imefanyika kwa Siku tano katika uwanja wa JK Park Jijini Dar es Salaam.