TANZANIA YAIBUKA VINARA MICHUANO YA MPIRA WA MIKONO UFUKWEN
service image
26 Feb, 2024

Klabu ya JKT na Kwale ya Kenya wamefanikiwa kuibuka mabingwa wa Mashindano ya Mpira wa Mikono Kanda ya Tano Afrika Mashariki kwa Vilabu yaliyofanyika kwenye Fukwe ya Coco Dar es Salaam Februari 23 na 24, 2024.

JKT kwa wanawake iliibuka na ushindi baada ya kuifunga kwa magoli ya penalty 5_4 timu ya Polisi Uganda, huku upande wa wanàume kwale ikishinda kwa penalty 2_1 dhidi ya Kilifi kutoka huko huko nchini kenya

Akizungumza baada ya mchezo kuisha Kocha Mkuu wa JKT Lidya Kimaro, alisema kujituma na kufuata maelekezo aliyowapa ndio siri ya ushindi wao pamoja na sapoti ya Viongozi.

"'kwa kweli Mimi kocha nilipambana na kuwapa mazoezi asubuhi, mchana na jioni Ili kuhakikisha tunafanya vizuri na malengo yametimia," alisema Lidya.

Kuhusu kuelekea kimataifa alisema kuwa watajipanga vyema Ili kuhakikisha wanakwenda kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika ambayo yatafanyika Juni mwaka huu.

Naye Nahodha wa JKT Zainabu Mohamed, alisema kuwa uzoefu wa kufanya mazoezi ya ufukweni ndio siri ya kutwaa ubingwa huo na kupongeza kuwa pamoja na kuibuka na ushindi huo, mchezo ulikuwa mgumu dhidi ya wapinzania wao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama Mpira wa mikono Tanzania (TAHA) Michael Martin Chibawala, aliwapongeza washindi na kusema mashindano ya 2025 yatafanyika kwa ukubwa zaidi.

Alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo mashindano hayo zilipaswa kushiriki nchi 10 katika nchi za Afrika Mashariki lakini zimeshiriki nchi tatu kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ukata wa fedha.

"Tanzania tumeonyesha uwezo wetu kufanikisha kuchukua Ubingwa kwa upande wa wanawake, pamoja kuwa mara ya kwanza kufanyika hapa nchini, "alisema Chibawala