Wanamichezo Tanzania Kunolewa na Watalaamu Kutoka Cuba
WANAMICHEZO TANZANIA KUNOLEWA NA WATAALAMU KUTOKA CUBA
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Osvaldo Vento Montiller Novemba 10, 2024 Jijini Havana .
Viongozi hao pamoja na mambo mengine wamejadili juu ya kuanzisha mashirikiano katika sekta ya michezo hususani mchezo wa Ngumi na Riadha (Mbiofupi, Miruko na mitupo).
Kwa upande wa ngumi wamesema kuwa, watabadilishana uzoefu kwa makocha wa mchezo huo kutoka Cuba kufundisha mabondia wa Tanzania kufuatia hatua iliyopigwa na taifa hilo katika mchezo huo unaokua kwa kasi nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bi. Fatma Rajab, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bi. Neema Msitha na viongozi wengine wa Wizara.