TANZANITE YAZIDI KUPAMBA MOTO

Tamasha la kimataifa la michezo kwa wanawake (Tanzanite) linafikia tamati kesho kwa kuwepo michezo wa soka la wanawake huku kukitarajiwa kuwepo kwa Derby kati ya Simba Queens dhidi ya Yanga Princess.
Tamasha hilo limeandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa lengo la kuongeza hamasa kwa wanawake nchini kushiriki michezo kwa wingi.
Mechi hiyo itatanguliwa na mtanange utakaopigwa mapema asubuhi kati ya Fountain gate dhidi ya Baobab Queens ya Dodoma michezo yote itachezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Tamasha la mwaka huu linalofanyika kwa siku tatu lilianza rasmi Alhamisi Oktoba 20, 2022, ambalo limehusisha michezo ikiwemo Riadha, Kabbadi, Karate, Jadi , Wavu, Kikapu kwa pande zote, mpira wa mikono, Netiboli na wanyanyua vitu vizito huku mchezo wa ngumi ukisubiriwa usiku wa leo Oktoba 21.