TEMBO WARRIORS WAFUZU FAINALI.
12 Sep, 2025
Timu ya Taifa ya Mpira ya miguu kwa watu wenye ulemavu (Tembo Warriors) imetinga hatua ya fainali ya mashindano ya Afrika Mashariki na kati ya mpira wa watu wenye ulemavu (CECAAF) baada ya ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Burundi ambao ni wenyeji wa mashindano yanayofanyika katika Jiji la Bunjumbura.

