TEMBO WARRIORS WAENDELEA KUJINOWA NCHINI UTURUKI

28 Sep, 2022
Timu ya Taifa ya Soka kwa Walemavu, Tembo Warriors leo Septemba 28, 2022 wameendelea na maandalizi yao wakiwa kambi maalum nchini Uturuki waliyoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya Oktoba Mosi kuanza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Hispania mjini Pendik.
Mazoezi hayo yameshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi ambaye amewasili nchini humo Septemba 27, 2022 pamoja na viongozi wengine wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki.