TEMBO WATAKIWA KUJITUMA NA KUONYESHA NIDHAMU
service image
13 Sep, 2022

Wachezaji wa timu ya ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu ya 'Tembo warriors' wametakiwa kupambana kwa ajili yao pamoja na nchi huku wakisisitizwa kuzingatia nidhamu katika kipindi chote cha mashindano.

Tembo Warrios inatarajia kuondoka kesho Septemba 14, 2022 kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kabla ya ufunguzi wa mashindano ya fainali za kombe la Dunia zitakazoanza Septemba 30 hadi Oktoba 9 mwaka huu.

Akizungumza Wakati wa kuiaga na kuikabidhi bendera timu hiyo kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leordigar Tenga, aliwaambia kuwa wakionyesha nidhamu nzuri dunia nzima itawaona.

"Mkionyesha nidhamu dunia nzima itawaona,"alisema Mwenyekiti Tenga.

Alisema kuwa, ombi la kujulikana kwa Tanzania ili watu waje, dhamana hiyo mmeibeba.

"Watanzania wanatamani kuona kila Mchezo unafanya vizuri, hivyo muende mkapambane, nchi ipo nyuma yenu, watanzania wanawaombea mkifanya vizuri ni ushindi wa nchi kwa ujumla," alisema Tenga.

"Mlituheshimisha Sana sio jambo dogo mkawaambukiza dada zenu wadogo mnakwenda hatua ya mwisho ya Kombe la dunia, matumaini yetu mtaendelea kwenda kutuheshimisha na matarajio ya watanzania, na lengo sio kufikia kombe la Dunia ni kurudi na ushindi Sasa mnayo dhamana kubwa," aliongeza Tenga.

Naye Nahodha wa timu hiyo Juma Kidevu kwa niaba ya tembo warriors wameahidi kwa Rais na watanzania hawatawaangusha ushindi ni dhamira yao.