KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA FILBERT BAY UWEKEZAJI KWENYE MICHEZO.
service image
17 Mar, 2024

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Machi 17, 2024 imefanya ziara katika Taasisi ya Filbert Bay iliyoko Kibaha Mkoani Pwani, ambayo inajihusisha na uwekezaji, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji vya michezo na kutoa pongezi kutokana na uwekezaji huo.

Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Musa Sima, imetoa pongezi hizo baada ya kuona uwekezaji uliofanywa katika ujenzi wa uwanja wa ndani wa michezo, viwanja vya nje, kituo Cha Afya, shule ya sekondari pamoja na hostel za wageni.

Mwekezaji Filbert Bayi aliwahi kuwa mwanariadha bora hapa nchini, na kusaidia kupatikana kwa wanariadha wengi wanaoitangaza vyema Tanzania pamoja na kuibua vipaji vya mchezo wa riadha ambavyo vinafanya vizuri mara kwa mara katika mashindano ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA).

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Nicholas Mkapa wameshiriki ziara hiyo pamoja na baadhi ya Viongozi wa wizara.