TOENI ELIMU KWA VIJANA WAFAIDIKE NA FURSA ZA TAASISI ZENU
service image
11 Oct, 2022

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Batrobas Katambi ni mmoja katika Viongozi waliofika katika banda linalohusisha taasisi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwemo Baraza la michezo la Taifa (BMT), Basata na Tasuba kupewa ufafanuzi wa majukumu yanayoendeshwa na taasisi hizo.

Mhe. Katambi amefika leo Oktoba 11, 2022 katika banda la taasisi za wizara yenye dhamana ya michezo wakati akikagua mabanda ya wadau mbalimbali kuelekea kesho kwenye ufunguzi wa wiki ya vijana, huku akiwataka maafisa wa taasisi hizo kutoa elimu ya kutosha kwa vijana ili wafaidike na fursa zilizopo katika taasisi hizo.