UBALOZI WA TANZANIA - MISRI

20 May, 2024
Balozi wa Tanzania nchini Misri Meja Gen. Richard Mutayoba Makanzo aahidi kuwepo pamoja washangiliaji wakutosha leo Mei 20, 2024 katika mechi ya kwanza ya Timu ya Taifa ya Mpira wa miguu ya watu wenye Ulemavu (Tembo Warriors) dhidi ya Sierra Leone itakayochezwa saa 12:30 jioni kwa saa ya Cairo sawa na Tanzania, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Petrosport nchini Misri.
Balozi, Mej. Jenerali Mutayoba pamoja na uwepo wake Cairo, Misri anahudumu pamoja na nchi za Lebanon, Palestina, Libya, Iraq, Syria na Jordan.