WASIMAMIZI WA VYUO VIKUU NA WAZAZI WAONE UMUHIMU WA KUIPA NGUVU MICHEZO
24 Jul, 2023
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha ametoa rai kwa Wasimamizi wa vyuo vikuu na Wazazi kuona umuhimu wa kuipa nguvu michezo katika maeneo yao ili iwe fursa kwa wanachuo na watoto wao kujiajiri kupitia vipaji vyao badala ya kusubiri kuajiriwa kupitia elimu peke yake.
Rai hii ameitoa leo Julai 24, 2023 wakati akiwaaga na kuwakabidhi bendera wachezaji wawili, mwogeleaji Naomi Samwel Amos kutoa Chuo kikuu cha Ardhi na mwanariadha Patrick Rwechugura kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya vyuo vikuu yanatarajiwa kuanza Julai 28 hadi Agosti 08, 2023 nchini China.