WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUIUNGA MKONO SERENGETI GIRLS
service image
26 Oct, 2022

Watanzania wametakiwa kuiunga mkono timu ya mpira ya wanawake umri chini miaka 17 (Serengeti Girls) kwa kuendelea kuichangia ili kuipa hamasa ya kufanya vizuri zaidi pamoja na kuipa heshima kwa kuiheshimisha nchi kufuzu kushiriki kombe la dunia lakini pia kufika hatua ya robo fainali katika mashindano ya kombe la dunia U-17 nchini India.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 26 na Mtangazaji Mkongwe wa RTD kwa sasa TBC Mbazingwa Hassan ambaye amefika Baraza la Michezo la Taifa kuonyesha mchango wake aliochangia kwa Serengeti Girls kupitia akaunti ya BMT huku akitoa wito kwa wadau wa maendeleo ya michezo na watanzania kuona mchango wa wasichana hao kwa taifa kwa kuendelea kuwapa hamasa ili waendelee kulitangaza taifa kwa kufanya vyema katika mashindano mbalimbali ya kimataifa watakayoshiriki.

"Nimewachangia elfu hamsini (50) dada zetu hawa na nitaendelea kuwachangia, watanzania tuendelee kuwaunga mkono wametuheshimisha sana kufika kombe la dunia kitu ambacho hakijawahi kutokea nchini,"alisema Mbazigwa.