WATER COM YAIUNGA MKONO SERIKALI KUELEKEA CHAN 2024
service image
30 Jul, 2025

Katibu Mtendaji wa Baraza la michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha ameipongeza kampuni ya vinywaji water com kwa kuungana mkono serikali kuelekea michuano ya CHAN 2024 kwa kufadhili maji yatakayotumika katika michuano hiyo.

Akipokea ufadhili huo leo Agosti katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam ameyakaribisha makampuni mbalimbali kuiunga mkono serikali katika michuano hiyo.

“Niseme kwa uwazi kuwa walichokitoa sio udhamini ni ufadhili kwa hiyo wamejiskia wawe sehemu ya kufanikisha jambo hili, kwa niaba ya serikali niwashukuru sana na nitoe wito kwa makampuni mengine kuiga mfano huu wa kizalendo kwa kuwa ni suala la nchi ni suala la wote na wao wawe sehemu ya kufanikisha jambo hili” Amesema Bi Neema Msitha

Kwa upande wake Meneja Mauzo kutoka Water com Bwan. Gidion Ngereza amesema kampuni hiyo ipo bega kwa bega na serikali kuwa sehemu ya kufanikisha michuano hiyo ufadhili huo unakuja ikiwa zimesalia siku 4 pekee kufunguliwa rasmi michuano ya CHAN 2024 ambapo mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya mwenyeji Tanzania na Bukinafaso katika dimba la Benjamini Mkapa majira ya saa mbili usiku.