YASHUSHI ATAKA WENYE ULEMAVU KUSHIRIKI LADIES FIRST
                            
                                
                                     22 Jan, 2023
                                
                            
                            Balozi wa Japan nchini Tanzania Maisawa Yasushi amewashauri waandaaji wa mashindano ya riadha ya wanawake (Ladies First) kuwa na utaratibu wa kuwahusisha wanamichezo wenye ulemavu.
Rai hiyo ameitoa leo tarehe 22 Januari, 2022 wakati wa hotuba yake ya ufungaji wa mashindano hayo ya riadha ya wanawake (Ladies First 2023) yaliyotamatika hii leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

