BMT, SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIKONO WAKAA KUJADILI...

BMT, SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIKONO WAKAA KUJADILI MAENDELEO YA MCHEZO

21 Sep, 2026
BMT, SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIKONO WAKAA KUJADILI MAENDELEO YA MCHEZO

 

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo tarehe 21 Septemba, 2026 limefanya kikao na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Mikono Tanzania (TAHA) kwa lengo la kujadili maendeleo na mikakati ya kuimarisha mchezo huo nchini.

Kikao hicho kimejadili, mambo mengi ya ukiwemo mikakati ya kumalizia mwaka 2026, maandalizi ya mashindano pamoja na programu za mafunzo kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa mpira wa mikono.

Kikao kimeongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Michezo BMT, Bw. Benson Chacha, ambaye amewapongeza viongozi wa Shirikisho hilo kwa juhudi wanazozifanya katika kuhakikisha mchezo wa mpira wa mikono unaendelea kukua na kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Shirikisho hilo limewakilishwa na Rais Michael Chibawala, Katibu Mkuu Yehoshefati Kalulu na Mjumbe Anna Kassiga.