Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limevitaka vyama vya michezo nchini kuandaa mafunzo na mashindano ya mara kwa mara kwa lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana, likitoa mfano wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA).
Wito huo umetolewa na Ofisa Michezo Mwandamizi wa BMT, Charles Maguzu, wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuogelea ya siku mbili yaliyoanza leo, Oktoba 10, 2026, katika Bwawa la Shaban Robert, Upanga, jijini Dar es Salaam.
Maguzu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya vyama vya michezo, wazazi na makocha katika kuandaa programu endelevu za kukuza vipaji vinavyoibuliwa kupitia mashindano hayo, ili kuwajengea vijana uwezo wa kushindana na kufanya vizuri katika mashindano yajayo.