Mwanariadha wa Tanzania Emmanuel Giniki Gisamoda amefanikiwa kushinda medali ya shaba katika mashindano ya mbio za Münster, zilizofanyika nchini Ujerumani tarehe 13 Septemba 2026.
Gisamoda amefikia mafanikio hayo baada ya kutumia muda wa saa 2:12:37, akifanya vizuri na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya kimataifa.
Ushindi huo unaendelea kuonyesha uwezo na ushindani wa wanariadha wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
Hongera Emmanuel Giniki Gisamoda kwa mafanikio haya na kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania