Hatua ya mtoano ya Ligi ya Taifa ya Mpira wa Wavu iliendelea Septemba 15, 2026, katika viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam, kwa michezo ya Robo Fainali kwa upande wa wanaume.
Katika michezo hiyo, Tanzania Prisons iliifunga JKT kwa seti 3-1, huku Jeshi Stars ikiibuka na ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Milambo VC.
High Voltage nayo ilipata ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Nyika VC, wakati Bandari ikiifunga KIUT kwa seti 3-0.
Matokeo hayo yameziwezesha Tanzania Prisons, Jeshi Stars, High Voltage na Bandari kutinga hatua ya Nusu Fainali, zikipambania nafasi ya kucheza Fainali.