GABRIEL GEAY ASHINDA MEDALI YA SHABA BERLIN MARATH...

GABRIEL GEAY ASHINDA MEDALI YA SHABA BERLIN MARATHON 2026

27 Sep, 2026
GABRIEL GEAY ASHINDA MEDALI YA SHABA BERLIN MARATHON 2026

 

Mwanariadha wa Tanzania, Gabriel Gerald Geay, ameandika historia katika Berlin Marathon 2026 baada ya kumaliza mbio hizo katika nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2:03:59 zilizofanyika leo tarehe 27 Septemba, 2026 Berlin, Ujerumani.

Geay ameonyesha kiwango cha juu na ushindani mkali katika mbio hizo, akifanikiwa kumaliza nyuma ya Guye Adola wa Ethiopia, aliyeshinda kwa muda wa saa 2:02:51, na Gemechu Dida Diriba, aliyeshika nafasi ya pili kwa saa 2:03:19.

Nafasi ya tatu ya Geay ni hatua muhimu kwa riadha ya Tanzania katika moja ya marathon kubwa na maarufu duniani.

Hongera Gabriel Geay kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania