Wahitimu wa Kozi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Michezo Hatua ya Kwanza wametakiwa kutumia elimu na ujuzi walioupata kuchangamkia fursa zitokanazo na michuano ya AFCON 2027. Hayo yamesemwa na Afisa Michezo Mwandamizi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bw. Charles Maguzu, leo Septemba 30, 2026, alipokuwa akifunga kozi hiyo iliyofanyika kwa siku tano katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuandaliwa na Mobile Sports Agency.
Aidha, akieleza kuwa ujuzi wa usimamizi na uendeshaji wa michezo unahitajika katika maandalizi na uendeshaji wa mashindano makubwa, ikiwemo maandalizi ya michuano ya AFCON 2027.
Vilevile, akizungumza wakati wa kufunga kozi hiyo, Maguzu aliwataka wahitimu pia kutumia elimu na ujuzi walioupata katika kuendeleza michezo, kubuni vyanzo vya mapato na kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta hiyo.
Aidha, aliwahimiza kuwa wabunifu na kuongeza ushirikiano na wadau mbalimbali, huku wakitumia ujuzi wao kuimarisha ushiriki wa watu wenye ulemavu na wasichana katika michezo.
“Katumieni elimu mliyopata katika kuendeleza michezo, kutumia ujuzi wenu kutengeneza vyanzo vya mapato na kuwa wabunifu katika maeneo yenu,” alisema Maguzu.
Kozi hiyo imelenga kuwaongezea washiriki maarifa na ujuzi wa usimamizi wa michezo, pamoja na kuwajengea uwezo wa kutumia taaluma hiyo katika kuimarisha maendeleo ya michezo na kuibua fursa mbalimbali kupitia sekta hiyo.