MASHINDANO YA MICHEZO YA MAJESHI KUFANYIKA MWANZA

MASHINDANO YA MICHEZO YA MAJESHI KUFANYIKA MWANZA

21 Sep, 2026
MASHINDANO YA MICHEZO YA MAJESHI KUFANYIKA MWANZA

 

Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) limeandaa Mashindano ya Michezo ya Majeshi yatakayofanyika Mwanza kuanzia Septemba 21 hadi Oktoba 5, 2026, yakishirikisha vikundi saba vya majeshi.

Mashindano hayo yatafanyika katika viwanja vya CCM Kirumba, SAUT, Butimba na Nyamagana, yakilenga kuimarisha ushindani na maendeleo ya michezo miongoni mwa wanamichezo wa majeshi.

Mwenyekiti wa BAMMATA, Meja Jenerali Said Hamis Said, amesema mashindano hayo hufanyika kila mwaka kwa kuzingatia mpango wa maandalizi wa BAMMATA na kwa lengo la kukuza sekta ya michezo nchini.

Kuelekea michuano hiyo, BAMMATA leo Septemba 20, 2026, limefanya Mbio za Pole (Jogging) za Mshikamano kati ya Majeshi na Wananchi katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, chini ya kaulimbiu:

“BAMMATA 2026: Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kudumisha Amani.”