Timu ya Taifa ya Wanaume U20 Ngorongoro Heroes itashuka dimbani leo, Septemba 22, 2026, kukabiliana na Burundi katika mchezo wa nusu fainali ya kuwania kufuzu AFCON U20 2027 – Kanda ya CECAFA.
Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Ngorongoro Heroes imefika hatua hii baada ya kuifunga Rwanda 3-0 na Ethiopia 4-0 katika hatua ya makundi.
BMT inaitakia kila la heri Ngorongoro heroes.