WALIMU SABA WA JUDO TANZANIA WANUFAIKA NA KOZI YA...

WALIMU SABA WA JUDO TANZANIA WANUFAIKA NA KOZI YA KIMATAIFA BURUNDI

10 Oct, 2026
WALIMU SABA WA JUDO TANZANIA WANUFAIKA NA KOZI YA KIMATAIFA BURUNDI

Walimu saba wa Judo kutoka Tanzania wameshiriki Kozi ya Kimataifa ya Uamuzi na Ualimu wa Judo iliyohitimishwa leo, Oktoba 10, 2026, nchini Burundi.

Kozi hiyo iliyoanza Oktoba 5, 2026, imeendeshwa na wataalamu kutoka Shirikisho la Kimataifa la Judo (IJF), ikishirikisha washiriki kutoka Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Tanzania na Uganda.

Mafunzo hayo yamelenga kuongeza maarifa na ujuzi wa walimu na waamuzi, kuboresha viwango vya ufundishaji na uamuzi, pamoja na kukuza ushirikiano na kubadilishana uzoefu kati ya nchi hizo.

Ushiriki wa Tanzania unatarajiwa kuimarisha maendeleo ya Judo nchini kupitia upatikanaji wa wataalamu wenye uwezo wa kutoa mafunzo yanayozingatia viwango vya kimataifa.