Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamond, ameendelea na maandalizi ya timu kuelekea Mashindano ya AFCON 2027, akilenga kujenga kikosi imara kupitia mafunzo na ushiriki katika michezo ya kimataifa.
Kocha Gamondi amekaa na timu Septemba 20, 2026 kuwapa mipango na kuweka nao mikakati mbalimbali kuelekea mafanikio katika Michuano hiyo.
Katika maandalizi hayo, Taifa Stars itacheza michezo miwili ya kufuzu AFCON 2027, ikianza dhidi ya Guinea-Bissau Septemba 25, 2026, katika Uwanja wa Amani, Zanzibar, kabla ya kukutana na Madagascar Septemba 29, 2026, nchini Morocco.
Aidha, timu hiyo itatumia dirisha hilo kujiandaa zaidi kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ghana Oktoba 4, 2026, utakaofanyika Casablanca, Morocco.
Maandalizi hayo ni sehemu ya mpango wa kujenga kikosi chenye ushindani na kujiandaa vyema kwa AFCON 2027.