Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Umri wa Chini ya Miaka 20 (AFCON U20) kwa Kanda ya CECAFA, yatakayoanza leo, Septemba 15 hadi 24, 2026, katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Tanzania ‘Ngorongoro Heroes’, ambao ni wenyeji na mabingwa watetezi, wapo Kundi A pamoja na Ethiopia na Rwanda. Kundi B linaundwa na Uganda, Sudani na Djibouti, huku Kundi C likiwa na Sudani Kusini, Kenya na Burundi.
Katika michezo ya leo, Uganda itakutana na Djibouti, huku Sudan Kusini ikichuana na Burundi.
Kwa upande wa wenyeji, Ngorongoro Heroes itashuka dimbani kukutana na Rwanda, huku ikilenga kuanza vyema safari ya kutetea ubingwa huo mbele ya mashabiki wa nyumbani.
Kila la heri Ngorongoro Heroes kuipeperusha vyema bendera ya Taifa.