TANZANIA U20 YAFUZU AFCON 2027, YAINGIA FAINALI YA...

TANZANIA U20 YAFUZU AFCON 2027, YAINGIA FAINALI YA CECAFA

22 Sep, 2026
TANZANIA U20 YAFUZU AFCON 2027, YAINGIA FAINALI YA CECAFA

 

Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (U20) 'Ngorongoro Heroes' imefuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana, AFCON U20, zitakazofanyika nchini Ghana mwaka 2027.

Ngorongoro Heroes imepata tiketi hiyo baada ya kutinga hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA U20, kufuatia ushindi wa mabao 2–0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Burundi katika mchezo wa nusu fainali.

Ushindi huo umeiwezesha Tanzania kufuzu na kupata nafasi ya kuiwakilisha Kanda ya CECAFA katika michuano ya AFCON U20 mwaka 2027.

Katika hatua ya fainali ya CECAFA U20, Tanzania itakutana na Sudan katika mchezo wa kuwania ubingwa wa michuano hiyo uliochezwa leo tarehe 22 Septeamba, 2026 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Kufuzu kwa Tanzania kushiriki AFCON U20 ni hatua muhimu katika safari ya maendeleo ya soka la vijana nchini, huku kikosi hicho kikipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake kwenye jukwaa kubwa la soka la Afrika.