MAKOCHA 29 MPIRA WA WAVU WAFAIDIKA NA MAFUNZO SINGIDA

Makocha 29 wa mchezo wa wavu kutoka mikoa mbalimbali wamefaidika na Mafunzo ya Daraja la kwanza ya ukocha yaliyoanza tarehe 2 na kuhitimishwa April 7, 2025 Mkoani Singida.
Mafunzo hayo yameendeshwa na mkufunzi kutoka Shirikisho la Mpira wa wavu Tanzania (TVF) Ford Edward.
Ofisa habari wa TVF Kepha Malecela amesema kuwa mafunzo hayo ni ya awali ambayo huwa yanafanyika ili kumuandaa mtu yoyote mwenye sifa ya kozi husika kuja kuwa mwalimu mzuri au kocha mzuri wa mchezo huo.
Amesema kuwa walengwa wa kozi hiyo ni mtu mwenye uzoefu wa mchezo wa mpira wa wavu ili apewa elimu akaandae wanafunzi wake ili kuwa wachezaji tegemewa wa baadaye.
"Kozi zetu zote na hii ikiwemo inajumuisha mtu yoyote mwenye sifa ya kozi husika, hivyo mtu yoyote mwenye vigezo kutoka sehemu yoyote ile anaruhusiwa kwenda kushiriki kozi itayokuwepo," amesema Melecela
Kozi ya singida imejumuisha washiriki toka Pwani, Manyara, iringa, Tabora, Shinyanga na Dodoma.