MILIONI 57.9 KUPITIA KWA WACHEZAJI WALIOSHIRIKI AFCON YA KWANZA 1980 KUSAIDIA TIMU ZA TAIFA
service image
12 Jan, 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanikiwa kukusanya Shilingi za Kitanzania Milioni 57.9 zitakazosaidia timu za taifa kupitia mnada wa jezi za wachezaji wa zamani walioiwakilisha nchi kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Kombe la Afrika (AFCON 1980).

Fedha hizo zimepatikana katika Harambee maalum kwa timu za taifa iliyoendeshwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa tarehe 10 Januari, 2024 Jijini Dar es salaam.

Jezi hizo ni pamoja na ya Juma Pondamali iliyonunuliwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa thamani ya shulingi milioni 25, Jezi ya Marehemu Joel Bendera iliyonunuliwa na Mfuko wa hifadhi za Jamii wa Tanzania PSSSF kwa thamani ya shilingi milioni 11, Jezi ya aliyekuwa mfungaji wa timu hiyo Peter Tino iliyonunuliwa na Benki ya NBC kwa thamani ya shilingi Milioni 7.5

Nyingine ni jezi ya aliyekuwa Nahodha wa timu hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leodigar Chilla Tenga iliyonunuliwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) kwa shilingi milioni 6, Rashid Chama ambaye Jezi yake amenunuliwa kwa thamani ya Milioni 6.2 na Kampuni ya Ulinzi ya K4 na Juma Nkambi ambaye jezi yake imenunuliwa na Benki ya CRDB kwa thamani ya Milioni 2.2.