Katiba ya Vyama na Mashirikisho ya michezo nchini
service image
16 Aug, 2024

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameongoza kikao cha kupokea na kujadili taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa na kamati ya kuandaa mfano wa Katiba itakayotumiwa na Vyama na Mashirikisho ya michezo nchini, pamoja na Kamati maalumu ya mahusiano kati ya Serikali, vyama na mashirikisho ya michezo.

Kikao hicho kimefanyika Agosti 16, 2024 Jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Gerson Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Methusela Ntonda na baadhi ya Wakurugezi wa Idara na Wakuu wa Taasisi za wizara, kimejadili pia muundo na uwazi katika masuala ya fedha kwenye vyama na mashirikisho hayo.