KOZI YA USIMAMIZI WA JUU WA MICHEZO

21 Jan, 2025
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Leodigar Tenga amewataka wahitimu wa kozi ya usimamizi wa juu wa michezo kutumia elimu hiyo kuendeleza michezo na kuwasihi kutoishia hapo bali wajiendeleze zaidi.
Rai hiyo ameitoa baada ya kuwatunuku vyeti vya Diploma wahitimu 12 wa mafunzo hayo wakati wa Mahafali ya pili ya kozi hiyo yaliyoratibiwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), hafla iliyofanyika tarehe 21 Januari, 2025 katika ukumbi wa Hoteli ya Tiffany jijini Dar es salaam.