AHADI YA RAIS DKT. SAMIA KWA TAIFA STARS.

13 Jun, 2024
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akikabidhi hundi ya Shilingi milioni mia moja ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kapteni wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) Himid Mao ikiwa ni ahadi aliyoitoa baada ya kushinda goli 1- 0 dhidi ya timu ya taifa Zambia (Chipolopolo) mchezo wa kufuzu kombe la dunia uliochezwa Juni 11, 2024 katika uwanja wa wa Levy Mwanawasa Ndola Nchini humo.