Mashindano ya Mataifa Afrika
service image
28 Nov, 2023

Mashindano ya Mataifa Afrika

Kikao cha kwanza cha maandalizi ya mashindano ya mataifa ya Afrika (All African Games) kimefanyika leo tarehe 28 Novemba, 2023 katika ukumbi wa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimeshirikisha baadhi ya watendaji wa wizara yenye dhamana ya michezo, Baraza la Michezo la Taifa na viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini.

Mashindano ya All African Games yanatarajiwa kufanyika mwezi Machi 2024 nchini Ghana.