BMT NA UFARANSA WANUIA KUSHIRIKIANA KATIKA KUENDELEZA MICHEZO
service image
19 Dec, 2023

Kaimu Meneja wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa Benson Chacha kwa niaba ya Katibu Mtendaji leo Disemba 19, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Etienne Pellausy ambaye ni Afisa Utamaduni na Michezo kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania wakilenga kushirikiana katika kuendeleza michezo nchini.

Aidha, katika mazungumzo yao Ufaransa wamekubali kuleta mtaalamu wa miradi anayetarajiwa kufanya kazi na BMT kwa miaka miwili kuanzia Januari 2024.

Culture and sport officer
French embassy in Tanzania