SERIKALI YAZIPONGEZA TIMU ZA TAIFA KUFIKIA HATUA MBALIMBALI ZA MASHINDANO KIMATAIFA
service image
04 May, 2026

Serikali imezipongeza timu mbalimbali za taifa nchini kutokana na mafanikio waliyopata ya kufikia hatua mbalimbali za mashindano ya kimataifa ikiwamo Timu ya Taifa ya mpira wa miguu “Taifa Stars” iliyofikia hatua ya 16 bora katika mashindano ya AFCON 2025 yaliyofanyika nchini Morocco na kufika hatua ya robo fainali ya mashindano ya CHAN 2024.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Mhe. Paul Makonda (MB), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 na kuongeza kuwa Timu ya wanawake ya Futsal ilishiriki Kombe la Dunia 2025 nchini Ufilipino na kufika hatua ya makundi, “Twiga Stars” ilitwaa ubingwa wa CECAFA Senior Women’s Championship 2025 na kufuzu WAFCON 2026, pamoja na timu ya mpira wa miguu kwa wenye ulemavu (amputee football) kwa ilishiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati nchini Burundi.

“Wizara inatoa pongezi kwa timu ya Taifa ya ngumi kwa kushinda jumla ya medali 18 (dhahabu 1, fedha 4 na shaba 13) katika mashindano ya kanda ya tatu Afrika yaliyofanyika Kenya mwaka 2025; timu ya mpira wa kikapu ya Dar City iliyoshiriki mashindano ya kikapu Afrika yaliyofanyika nchini Afrika Kusini na kufanikiwa kufuzu kucheza fainali ya mashindano hayo itakayofanyika nchini Rwanda Mei 2026” amesisitiza Mhe. Makonda.

Aidha, amewapongeza bondia Ibrahim Class aliyepigana na kupata mikanda miwili ya WBC na WBO, bondia Lupakisyo Shoti aliyeshinda mkanda wa IBO Afrika, Amani Bariki (Manichuga) aliyeshinda mkanda wa WBC Intercontinental, Frank Shagembe aliyeshinda mkanda wa WBO Afrika kwa uzito kilo 90, Yusuph Changarawe aliyeshinda mkanda wa WBC Afrika na Halima Vunjabei aliyeshinda mkanda wa PST.

slot gacor