KATIBU MTENDAJI WA BMT ATEMBELEA KAMBI YA TWIGA STARS
service image
26 Nov, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha, leo tarehe 26 Novemba, 2023 ameitembelea Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) iliyoweka kambi katika hotel ya Aura Suites Jijini Dar es Salaam, ikijiandaa na mchezo wa mwisho kufuzu WAFCON dhidi ya Timu ya Taifa ya Togo utakaochezwa Novemba 30 Chamazi Complex na Disemba 5 nchini Togo.